Deuteronomy 27:13-18

13 aMakabila haya yatasimama juu ya Mlima Ebali kwa kutamka laana: Reubeni, Gadi, Asheri, Zabuloni, Dani na Naftali.

14 bNao Walawi watawasomea watu wote wa Israeli kwa sauti kubwa:

15

c“Alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga au mwenye kusubu sanamu, kitu ambacho ni chukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi stadi, na kuisimamisha kwa siri.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

16

d“Alaaniwe mtu amdharauye baba yake na mama yake.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

17

e“Alaaniwe mtu asogezaye jiwe la mpaka wa jirani yake.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

18

f“Alaaniwe mtu ampotoshaye kipofu njiani.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

Copyright information for SwhKC